Vyombo vya Magharibi vyaakisi kwa wingi miongozo ya Kiongozi Muadhamu
Vyombo vya Magharibi vyaakisi kwa wingi miongozo ya Kiongozi Muadhamu Dec 12, 2024 06:31 UTC Mashirika ya habari ya nchi za Magharibi yameakisi kwa wingi hotuba na miongozo muhimu ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyotoa jana Jumano akisisitiza kuwa Marekani na utawala wa Kizayuni ni wahusika wakuu wa matukio ya Syria. Shirika la habari la Reuters la utawala wa kifalme wa Uingereza limeandika: (Ayatullah) Ali Khamenei Jumatano amesema, Iran ina ushahidi unaoonesha kuwa, kupinduliwa serikali ya Rais Assad wa Syria ni njama za Marekani na Israel na mmoja wa majirani wa Syria lakini hakutaja ni jirani gani huyo. Shirika hilo la habari limeendelea kuandika: Uturuki ambayo ni mwanachama wa NATO, ilikuwa inazikalia ardhi za kaskazini mwa Syria baada ya kufanya mashambulizi kadhaa dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi na (Erdogan) alikuwa mmoja wa waungaji mko...