Iran: Kuchaguliwa al Sinwar kunadhihirisha matumaini, umoja na nguvu ndani ya Hamas
Iran: Kuchaguliwa al Sinwar kunadhihirisha matumaini, umoja na nguvu ndani ya Hamas
Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa kuchaguliwa Yahya al Sinwar kuwa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) kunaonyesha umoja na uwezo wa harakati hiyo ya muqawama mkabala wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Baada ya kuuawa shahidi Ismail Haniyeh, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imemchagua Yahya Ibrahim al Sinwar kuwa Mkuu wa Ofsi ya Kisiasa ya harakati hiyo.
Ismail Haniyeh, aliyekuwa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas, na mlinzi wake waliuawa shahidi alfajiri ya Jumatano Julai 31 mwaka huu katika shambulio la kigaidi alipokuwa Tehran kushiriki hafla ya kuapishwa rasmi Rais mpya wa Iran.
Shirika la Habari la Iiran (IRNA) limeripoti kuwa, Ali Baqeri Kani Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran jana Alhamisi alimtumia ujumbe Yahya al Sinwar akimpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Mkuu mpya wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas.
Bagheri Kani amesema kuwa kuchaguliwa Sinwar wakati huu nyeti kunarejesha matumaini, umoja, nguvu na ushindi kwa harakati ya Hamas, wananchi wa Palestina na Mhimili wa Muqawama; na pia kunadhihirisha kukata tamaa na kushindwa sera za ugaidi, uvamizi na uchokozi za utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake kimataifa.
Comments
Post a Comment