Hofu hospitali za Gaza wakati mafuta na misaada vinapungua

Hofu hospitali za Gaza wakati mafuta na misaada vinapungua Sudi Mnette Saa 14 zilizopitaSaa 14 zilizopita Wizara ya afya ya Gaza imesema hospitali zimesalia na siku mbili tu za mafuta kabla ya kuzuia huduma, baada ya Umoja wa Mataifa kuonya kwamba utoaji wa misaada katika eneo lililoharibiwa na vita umetatizwa. https://p.dw.com/p/4nLjU Nakili kiunganishi Gaza Grenzübergang Rafah Mtoa tiba akimuhamisha mtoto mchanga njiti kutoka Ukanda wa Gaza katika eneo la kivuko cha Rafah Novemba 20, 2023. Picha: Egypt's State Information Center/Xinhua/picture alliance Matangazo Onyo hilo la wizara hiyo inayodhibitiwa na kundi la Hamasliimekuja siku moja baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kutoa hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na aliyekuwa waziri wa ulinzi Yoav Gallant ikiwa ni zaidi ya mwaka tangu kuanza kwa vita vya Gaza. Madaktari wa Gaza wamesema uvamizi wa Israel wa usiku wa kuamkia leo katika miji ya Beit Lahia na karibu na Jabalia ulisababisha idadi kadhaa ya watu kuuawa au kutoweka. Mara kwa mara Umoja wa Mataifa na mashiriki mengine ya misaada ya kiutu umeelezea hali ya kibinadamu, haswa kaskazini mwa Gaza, ambapo Israeli ilisema Ijumaa iliwaua makamanda wawili waliohusika katika shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023 ambalo ndio kiini cha vita.

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan