Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

 

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Mashirika yaliyotia saini Azimio la Machi 31 yamefanya mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatano, Novemba 20, kutaka wafungwa wote wa kisiasa waachiliwe. Haya yanajiri wakati mawaziri na viongozi 11 wa zamani wa vyama vya siasa wanaodai kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba wamekuwa kizuizini kwa zaidi ya miezi mitano. Wanachama wote wa jukwaa hili, wanashitakiwa kwa "upinzani wa utumiaji wa mamlaka halali", haswa.

Wito huo kutoka kwa watia saini wa Azimio la Machi 31 unakuja wakati mawaziri 11 wa zamani na viongozi wa vyama vya siasa wanachama wa jukwaa bado wako kizuizini, zaidi ya miezi mitano baada ya kukamatwa kwao. Hapa, ni moja ya mitaa ya mji wa Bamako, Aprili 2023.
Wito huo kutoka kwa watia saini wa Azimio la Machi 31 unakuja wakati mawaziri 11 wa zamani na viongozi wa vyama vya siasa wanachama wa jukwaa bado wako kizuizini, zaidi ya miezi mitano baada ya kukamatwa kwao. Hapa, ni moja ya mitaa ya mji wa Bamako, Aprili 2023. dpa/picture alliance via Getty I - picture alliance
Matangazo ya kibiashara

Wakati maombi ya kuachiliwa kwa muda kwa mawaziri 11 wa zamani na viongozi wa vyama wanachama wa Azimio la Machi 31 - yaliyokubaliwa na jaji - yalipata upinzani kutoka kwa upande wa mashtaka, upatanishi uliofanywa na mamlaka ya mpito haukufanikiwa.

Ni katika muktadha huu ambapo Mahamadou Konaté, rais wa vuguvugu la Rebuild-Baara ni Yiriwa na msemaji wa Azimio la Machi 31, siku ya Jumatano, Novemba 20, amefanya mkutano na waandishi wa habari.

"Ni muhimu zaidi kuwahutubia wananchi wenzetu ambao wamegundua kwamba, kwa muda wa miezi mitano, tulienda kwa mamlaka ya mpito bila majibu mazuri ili wenzetu 11 wa kisiasa, waliokamatwa kinyume na utaratibu wowote wa kisheria, wapate uhuru wao," amesema hasa kabla ya kuongeza: pia tunatoa wito kwa wakazi kushuhudia kwamba kuanzia leo, tunataka kuendeleza mapambano yetu kwa wafungwa wote wa kisiasa.”

Na msemaji wa mashirika yaliyotia saini Azimio la Machi 31 aliorodhesha majina ya Ras Bath, mwandishi wa safu ya redio na mwanaharakati wa mashirika ya kiraia, "Ben the brain", chama cha Yerewolo, Clément Dembélé, mwanaharakati wa kupambana na ufisadi, au hata "Rose vie cher. ”, mshawishi kwenye mitandao ya kijamii. "Hao si sehemu ya muungano wetu wa kisiasa," amesema Mahamadou Konaté, akiwaomba wananchi wa Mali "kujiunga" na mapambano ili "kukomesha msukumo huu wa kupindukia dhidi ya uhuru na haki za mtu binafsi."

Zaidi ya wito huu wa kuachiliwa kwa wafungwa wote wa kisiasa, mashirika ya Azimio la Machi 31, ambalo linaleta pamoja karibu vyama vyote vya kisiasa nchini, yanataka kuwashawishi wakazi kuhusika kwao katika masuala ya kijamii. "Hatujajali matatizo ya kila siku ya wananchi wote wa Mali: gharama kubwa ya maisha, ukosefu wa ajira ambao unaendelea kuongezeka kutokana na kufungwa kwa mamia ya biashara," almesema Mahamadou Konaté. Pia ametoa mfano wa “kukatika kwa umeme kupita kiasi kwa takriban miaka miwili” kabla ya kuhitimisha: “Ni kwa manufaa ya kila mmoja kusimama kama mtu mmoja kusema inatosha! ".

Muungano huo pia unaendelea kudai kufanyika kwa uchaguzi huru na wa wazi ili hatimaye kuwezesha- na kama ilivyoahidiwa na utawala uliokuwepo zaidi ya miaka minne iliyopita - kurejea kwa utaratibu wa kikatiba.

Comments

Popular posts from this blog

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan