Senegal: Chama cha rais Faye kimepata idadi kubwa ya viti vya ubunge

 

Senegal: Chama cha rais Faye kimepata idadi kubwa ya viti vya ubunge

Chama tawala nchini Senegal, Pastef, kimeshinda karibu robo tatu ya viti vya ubunge katika uchaguzi uliofanyika wikendi iliyopita, matokeo yanayomaanisha kuwa sasa sera za Serikali mpya zitapitishwa kirahisi.

Ikiwa ushindi huu wa chama cha Pastef utathibitishwa na mahakama, utakuwa ushindi mkubwa zaidi katika historia ya chaguzi za taifa hilo kwa chama kimoja kufikisha wabunge zaidi ya 120.
Ikiwa ushindi huu wa chama cha Pastef utathibitishwa na mahakama, utakuwa ushindi mkubwa zaidi katika historia ya chaguzi za taifa hilo kwa chama kimoja kufikisha wabunge zaidi ya 120. © Abdou Karim Ndoye / Senegal's Pres / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa matokeo ya awali, chama cha rais Bassirou Faye kimepata wabunge 130 kati ya 165 wanaotakiwa katika bunge la kitaifa, matokeo yaliyothibitisha na maofisa wa chama tawala.

Matokeo haya hata hivyo yatasalia kuwa ya awali hadi pale yatakapothibitishwa na mahakama ya kikatiba ndani ya siku 5 zijazo.

Rais wa Senegal  Bassirou Diomaye Faye, wakati akiwa na mtangulizi wake Macky Sall jijini Dakar tarehe 28, Machi 2024.
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, wakati akiwa na mtangulizi wake Macky Sall jijini Dakar tarehe 28, Machi 2024. © Présidence du Sénégal/document via REUTERS

Ikiwa ushindi huu wa chama cha Pastef utathibitishwa na mahakama, utakuwa ushindi mkubwa zaidi katika historia ya chaguzi za taifa hilo kwa chama kimoja kufikisha wabunge zaidi ya 120.

Upinzani uliokuwa unaongozwa na rais wa zamani Macky Sall, uliambulia wabunge 16, huku chama cha waziri mkuu wa zamani Amadou Ba kikipata viti 7 na viti vitatu vilienda kwa aliyekuwa meya wa Dakar Barthelemy Dias.

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan