Niger: Wapiganaji wapya zaidi ya mia moja kutoka makundi ya waasi wajisalimisha

 

Niger: Wapiganaji wapya zaidi ya mia moja kutoka makundi ya waasi wajisalimisha

Takriban wanachama mia moja wa makundi mawili ya waasi nchini Niger, moja lililoundwa kumuunga mkono Rais Mohamed Bazoum aliyepinduliwa na mapinduzi ya kijeshi na kutekwa na jeshi lililo madarakani, wamejisalimisha siku ya Jumatano, Novemba 27, imetangaza redio ya serikali iliyonukuliwa na shirika la habari la AFP.

Wanajeshi wa Niger wakitembea karibu na mabaki baada ya mashambulizi ya kujitoa mhanga huko Agadez, Niger.
Wanajeshi wa Niger wakitembea karibu na mabaki baada ya mashambulizi ya kujitoa mhanga huko Agadez, Niger. © AP
Matangazo ya kibiashara

"Wapiganaji zaidi ya mia moja wa chama cha Patriotic Liberation Front na Movement for Justice and Rehabilitation of Niger wameamua kuweka chini silaha zao, na hivyo kuashiria kurejea kwao kwenye uhalali," imesema Voix du Sahel.

Sherehe iliandaliwa huko Agadez, mji mkubwa kaskazini mwa Niger karibu na Libya, wakati ambapo waasi wa zamani walikabidhi "silaha kubwa za vita" na "karibu magari kumi na tano" kwa gavana wa eneo hilo, Jenerali Ibra Boulama, radio ya serikali imesema.

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan