Rais wa zamani Macky Sall analenga kurejea tena katika siasa za Senegal

 

Rais wa zamani Macky Sall analenga kurejea tena katika siasa za Senegal

Rais wa zamani wa Senegal Macky Sall, analenga kurejea tena katika ulingo wa kisiasa katika uchaguzi wa dharura wa wabunge ulioratibiwa kufanyika siku ya Jumapili.

Rais wa zamani wa Senegal Macky Sall , Tarehe 25 Oktoba 2023.
Rais wa zamani wa Senegal Macky Sall , Tarehe 25 Oktoba 2023. REUTERS - JOHANNA GERON
Matangazo ya kibiashara

Sall ambaye kwa sasa anaishi nchini Morocco, aliondoka madarakani mwezi Aprili mwaka huu baada ya kuongoza kwa kipindi cha miaka 12, akimuachia uongozi mrithi wake Bassirou Diomaye Faye.

Rais wa zamani kwa sasa anaongoza muungano mpya wa upinzani akiwa katika nchi ya kigeni, suala ambalo wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanahoaji nia yake ya kutaka kurejea tena kwenye siasa za taifa hilo la Afrika Magharibi.

Waziri Mkuu wa sasa wa Senegal, hasimu wa kisasa wa Sall, Ousmane Sonko, ameendelea kusisitiza kwamba wanasiasa wote waliokuwa katika utawala wa zamani huenda wakafunguliwa mashtaka.

Image Archive / Le président sénégalais sortant Macky Sall (à droite) rencontrant le président sénégalais élu Bassirou Diomaye Faye (à gauche) au palais présidentiel de Dakar, le 28 mars 2024.
Bassirou Diomaye Faye, Rais wa sasa wa Senegal na aliyekuwa mtangulizi wake Macky Sall. © Présidence de la République du Sénégal

Sonko amekuwa akiutuhumu utawala wa Sall kwa kuhusika na ubadhirifu wa pesa za umaa, madai ambayo hata hivyo viongozi wa zamani wametupilia mbali.

Mchambuzi na mtaalam wa masuala ya kisiasa professa Maurice Soudieck Dione anasema hatua ya Sall kurejea kwenye siasa ni njia moja ya kulinda masilahi yake iwapo kungetokea athari zozote za kisiasa dhidi yake.

Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye na Waziri Mkuu Ousmane Sonko Tarehe 15 Machi 2024.
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye na Waziri Mkuu Ousmane Sonko Tarehe 15 Machi 2024. AP - Sylvain Cherkaoui

Sall alihairisha uchaguzi mkuu wa urais wa mwezi Februari, hatua ambayo ilizua mzozo mkubwa wa kisiasa nchni Senegal. Licha ya Sall kumpendekeza Amadou Ba, kumrithi kwenye uchaguzi huo, mgombea wake alipoteza dhidi ya naibu wa zamani wa Sonko Faye.

Faye na Sonko waliachiwa kutoka gerezani siku kumi kabla ya uchaguzi mkuu wa urais. Rais Faye alivunja bunge ambalo lilikuwa na idadi kubwa ya wapinzani mwezi Septemba na kutoa nafasi ya kufanyika kwa uchaguzi mpya wa wabunge.

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan