Katika miezi tisa iliyopita Yemen imeshambulia meli 170 za Marekani na Wazayuni

 

Aug 08, 2024 06:32 UTC
  • Katika miezi tisa iliyopita Yemen imeshambulia meli 170 za Marekani na Wazayuni

Tovuti ya habari ya Yemen imetangaza katika ripoti yake kuwa katika kipindi cha miezi tisa iliyopita vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vimezishambulia meli 170 za Wamarekani na Wazayuni.

 Almasirah imeeleza katika ripoti yake iliyochunguza operesheni zilizofanywa na vikosi vya ulinzi vya Yemen kati ya Novemba 2023 hadi Julai mwaka huu kwamba katika operesheni hizo, vikosi hivyo vimezilenga meli zipatazo 170 zenye uhusiano na adui Mzayuni.
 
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, meli 41 kati ya zilizopigwa zilikuwa za adui wa Kizayuni, meli 72 za Marekani na meli 12 zilikuwa za Uingereza.
 
Ripoti hiyo imeongeza kuwa, kati ya hizo zote, karibu meli 45 zimeshambuliwa na jeshi la Yemen kutokana na kukiuka marufuku ya kuingia katika bandari za utawala wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina.

Almasirah imemalizia ripoti hiyo kwa kubainisha kuwa katika operesheni zake hizo, vikosi vya ulinzi vya Yemen vimeshambulia jumla ya vyombo 49 vya kivita zikiwemo manowari, meli za kivita za kushambulia, boti za kivita na meli za kubebea ndege za kivita.

 
Jeshi la Yemen ambalo limekuwa bega kwa bega na Wapalestina wa Ghaza tangu ulipoanza uvamizi na mauaji ya kimbari yanayofanywa na jeshi katili la Kizayuni dhidi ya Wapalestina hao; na likiwa hadi sasa limetiwa hasara kubwa kutokana na mashambulizi ya ndege za kivita za Marekani na Uingereza, limetangaza kuwa, operesheni za vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo dhidi ya meli za Israel au zinazoelekea bandari za utawala huo katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu zitasitishwa pale tu uvamizi na mzingiro waliowekewa watu wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza vitakapokomeshwa.
 
Wizara ya Afya ya Palestina imetoa ripoti mpya ya idadi ya Wapalestina waliouliwa shahidi na kujeruhiwa kutokana na jinai za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza na kueleza kuwa tangu yalipoanza mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Ghaza, hadi sasa watu elfu 39,677 wameuawa shahidi na wengine 91,645 wamejeruhiwa.../

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan