Muhammad Eslami: Sera za milango wazi zipo katika ajenda ya kazi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Muhammad Eslami: Sera za milango wazi zipo katika ajenda ya kazi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia ya Iran amesema kuwa nchi za Magharibi zinaituhumu Iran kuwa inaficha sekta yake ya nyuklia, ilhali Tehran inatekeleza sera za milango wazi katika ajenda yake.
Muhammad Eslami amesema kuwa nchi za Magharibi zinapinga maendeleo ya sekta ya nyuklia ya Iran na kwamba hivi sasa dawa aina 60 zinazalishwa nchini Iran kwa kutumia teknolojia ya nyuklia, na dawa nyingine 20 katika ziko katika majaribio ya kimatibabu.
Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia ya Iran alieleza haya jana Alhamisi katika Mkutano wa Taifa kuhusu Nafasi na Matumizi ya Teknolojia ya Nyukia katika Mfumo wa Afya".
Eslami pia aligusia jinai kubwa na za kikatili zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia wa Palestina wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza na kusema kuwa, walimwengu wametambua vyema kiwango cha jinai za Israel huko Gaza na Palestina kwa ujumla licha ya kukandamizwa vyombo vya habari; na sasa Palestina imekuwa suala kuu la ulimwengu mzima.
Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia ya Iran amesema, Israel haijatimiza hata lengo moja baada ya mashambulizi na mauaji yake ya kimbari ya miezi kadhaa sasa dhidi ya Gaza sambamba na kuendelea kulizingira eneo hilo.
Comments
Post a Comment