Ofisi ya Kudumu ya I.R.Iran UN: Iran itaifanya Israel ijutie uchokozi wa kigaidi iliofanya
Ofisi ya Kudumu ya I.R.Iran UN: Iran itaifanya Israel ijutie uchokozi wa kigaidi iliofanya
Aug 08, 2024 07:05 UTC
Ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa imesema Tehran itaufanya utawala wa Kizayuni wa Israel ujutie kitendo cha uchokozi wa kigaidi uliofanya hivi karibuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu uliopelekea kuuawa shahidi kiongozi mkuu wa Hamas, Ismail Haniya.
Ofisi hiyo ya uwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
katika UN ilitoa kauli hiyo jana Jumatano wakati wa kujibu masuali
kuhusu madai kwamba Tehran inaweza ikafuta kisasi chake ikiwa Tel Aviv
itafikia makubaliano na Hamas ambayo yataleta suluhu katika vita
vinavyoendelea vya utawala huo vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa
Ghaza.
"Tumekuwa tukifuatilia vipaumbele viwili kwa wakati mmoja,"
imeeleza ofisi hiyo ya uwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa na
kufafanua kwa kusema: "kwanza, kufikiwa usitishaji vita thabiti huko
Ghaza na kuondolewa wavamizi katika eneo hilo. Na pili ni kutoa adhabu
ya mvamizi kwa mauaji ya Shahidi Haniya, kuzuia kurudiwa kwa vitendo vya
uchokozi vya utawala wa Kizayuni, na kuwafanya Wazayuni wajutie kuingia
kwenye mkondo huu".
Mapema jana Jumatano, Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Ali Bagheri Kani alirudia na kutilia azma iliyonayo Jamhuri ya Kiislamu ya kuchukua hatua dhidi ya utawala wa Kizayuni.
Bagheri, ambaye alikuwa akihutubia kikao cha dharura cha Jumuiya ya
Ushirikiano wa Kiislamu OIC mjini Jeddah, Saudi Arabia alisema
Tehran haina chaguo jengine isipokuwa kulipiza kisasi dhidi ya utawala
huo kutokana na mauaji hayo na kuongeza kuwa hatua hiyo ni muhimu ili
kuzuia uchokozi zaidi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu wakati Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa limekaa bila ya kuchukua hatua yoyote.../
Comments
Post a Comment