Sergei Shoigu: Ushirikiano wa Tehran na Moscow unaongezeka
Sergei Shoigu: Ushirikiano wa Tehran na Moscow unaongezeka
Katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia amesema kuwa ushirikiano kati ya Tehran na Moscow unaendelea kupanuka.
Sergei Shoigu amehojiwa na televisheni ya Russia 24 na kueleza kuwa ushirikiano wa Tehran na Moscow unaendelea kuimarika na kwa kasi kubwa katika nyanja zote.
Shoigu ameongeza kuwa, katika mazungumzo aliyofanya hapa Tehran na Rais Masoud Pezeshkian na Ali Akbar Ahmadian Katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Iran wamebadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa pande mbili na pia hali ya mambo ya Syria na Lebanon.
Katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia pia ameshiria tukio chungu la kuuliwa kigaidi Ismail Haniyeh Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas mjini Tehran na kueleza kuwa suala hili haliwezi kupuuzwa hata kidogo.
Sergei Shoigu, Katibu wa Baraza la Usalama la Taifa la Russia sambamba na kushadidi mivutano ya utawala wa Kizayuni katika eneo hili, aliwasili mjini Tehran juzi kwa mwaliko wa Ali Akbar Ahmadian, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran. Shoigu akiongoza ujumbe wa ngazi ya juu wa Russia aliwasili Tehran kwa lengo la kuendeleza ushirikiano wa kistratejia kati ya nchi mbili ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa ngazi ya juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Comments
Post a Comment