Utendaji wa kiuadui wa Israel dhidi ya Iran na muqawama na athari hasi za kijamii katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu

 

  • Utendaji wa kiuadui wa Israel dhidi ya Iran na muqawama na athari hasi za kijamii katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu

Hali na mazingira ya kijamii katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) yapo kwa namna ambayo vitisho vya nje vitakuwa na uharibifu mkubwa na matokeo mabaya kwa jamii hiyo.

Jumatano iliyopita na katika kitendo kingine cha jinai, utawala wa kigaidi wa Kizayuni ulimuua shahidi Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS. Jinai hiyo ya kinyama ya Israel ilitekelezwa hapa mjini Tehran. Baada ya jinai hiyo, Kiongozi wa Muadhamu Mapinduzi ya Kiislamu alitangaza katika ujumbe wake akisema:

Utawala wa Kizayuni ambao ni mtenda jinai na ni utawala wa kigaidi, umemuua shahidi mgeni wetu kipenzi kwenye nyumba yetu na kututia majonzi makubwa, hivyo utawala huo umejiandalia mazingira ya kuadhibiwa vikali na tunaona kuwa ni wajibu wetu kulipiza kisasi cha damu ya shahidi huyo.

Kwa muktadha huo, msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni jibu kali kwa kitendo cha jinai cha Tel Aviv.

Juhudi za baadhi ya nchi za kieneo na magharibi za kuishawishi Iran isijibu au ijibu lakini kwa nguvu ndogo bado hazijazaa matunda.

Filihali kila mtu, wakiwemo Wazayuni, wanasubiri jibu la kali kutoka kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Subira ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na juhudi zake za kujibu kwa wakati mwafaka kumesababisha kudorora kwa hali ya kijamii katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu zilizopewa jina bandia la Israel. Kutokuweko uhakika wa kiusalama wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu kulisababisha mashirika 15 ya ndege ya kimataifa kusitisha safari zao za kuelekea Tel Aviv. Kusitishwa kwa safari za ndege pia kumezua hali ya kuchanganyikiwa watu juu ya  kurejea Tel Aviv na pia kuwafanya wasitesite kurejea huko.

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeripoti kuwa, takriban Waisraeli 150,000 wamekwama nje ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu kutokana na kusitishwa safari za ndege za kuelekea Tel Aviv. Usalama na ustawi zilikuwa ahadi mbili muhimu kwa Wayahudi za kuhamia katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. Lakini vita vya mara kwa mara ambavyo baraza la mawaziri la Netanyahu limekuwa likiendesha katika muongo mmoja uliopita, na hasa mauaji ya kimbari huko Gaza, ambayo yalikabiliwa na majibu ya makundi ya muqawama nayo pia ni sababu iliyoibua hofu na kihoro na kusababisha matatizo ya kiuchumi na hivyo kuwafanya kukata shauri la kuhama kutoka katika ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu.

Shahidi Ismail Hania

 

Mbali na masuala ya kiuchumi na kimaisha, usalama wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni umefichuliwa na kufahamika kuwa ni kelele za debe tupu lisilo na kitu ndani yake. Kama vile haitoshi, walowezi wa Kizayuni walioko Israel sio tu kwamba, hawajapata ustawi wa kiuchumi bali daima wanaoishi roho mkononi kutokana na hofu ya kushambuliwa na makombora ya muqawama na hivi sasa wana wahaka wa kukabiliwa na mashambulio ya makombora na ndege zisizo na rubani za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mambo haya na mengineyo yamewafanya walowezi hao kuchukua uamuzi wa kuzihama ardhi zinazokaliwa kwa mabavu hatua ambayo ni pigo kwa serikali ya Netanyahu na washirika wake.

Mbali na madhara hayo, sambamba na kushika kasi mvutano kati ya Tel Aviv na Iran na uwezekano wa kutokea shambulio la makombora na ndege zisizo na rubani za Iran katika kujibu na mauaji ya shahidi Ismail Haniyeh mjini Tehran yaliyofanywa na Israel, serikali mbalimbali za dunia zimewashauri rai wao kuondoka katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel na kutofanya safari za kwenda huko.

 

Suala hili pia ni dalili ya udhaifu wa kiusalama wa utawala wa Kizayuni hasa kwa kutilia maanani kwamba, hilo litapunguza  mapato ya utawala huo yanayotokana na utalii na hivyo kuuongezea utawala huo matatizo ya kiuchumi ambayo yamezidi kushadidi hasa katika kipindi cha miezi 10 iliyopita.

Nukta ya mwisho ni kwamba, iwapo hatua tarajiwa ya Iran dhidi ya Israel itakabiliwa na jibu la Israel na kuibuka vita vya siku kadhaa, madhara ya kijamii yanayotajwa kwa utawala wa Kizayuni yatakuwa makali zaidi. Matokeo haya yanasababishwa zaidi na ukweli kwamba, Israel ni utawala bandia wenye utambulisho wa watu wasio wa asili  ya ardhi hizo ambao kimsingi hawana utambulisho wa kitaifa.

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan