Blinken barani Ulaya kuunga mkono Ukraine baada ya uchaguzi wa Trump
Blinken barani Ulaya kuunga mkono Ukraine baada ya uchaguzi wa Trump
Mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken amesafiri kwa ndege kuelekea Brussels siku ya Jumanne kwa mazungumzo ya dharura na nchi za Ulaya katika jaribio la kuharakisha misaada kwa Ukraine kabla ya rais mteule Donald Trump kuingia madarakani.
Imechapishwa:
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani atakutana na maafisa wa NATO na Umoja wa Ulaya siku ya Jumatano "kujadili uungaji mkono kwa Ukraine katika utetezi wake dhidi ya uvamizi wa Urusi," msemaji wake Matthew Miller amesema katika taarifa.
Rais wa zamani wa Marekani (2017-2021), ambaye atarejea Ikulu mnamo Januari 20, ameanza kushughulikia sula hili.
Alizungumza na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky. Kulingana na Gazeti la Washington Post, pia alizungumza na Rais wa Urusi Vladimir Putin kumwomba kutozidisha mgogoro nchini Ukraine, habari hii hata hivyo ilikanushwa na Kremlin, ambayo ilizungumzia "habazi za uongo".
Donald Trump pia anajiandaa, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, kumteua seneta wa Florida mwenye ushawishi Marco Rubio kama waziri wake wa mambo ya nje. Hivi majuzi Marco Rubio alihisi kuwa vita vya Ukraine "lazima vikomeshwe".
- Kumaliza vita "kwa siku moja" -
Tajiri huyo mwenye umri wa miaka 78 amekuwa akidai mara kwa mara kuwa anaweza kumaliza vita "katika siku moja" hata kabla ya kuchukua madaraka, bila hata kueleza jinsi angefanya.
Lakini alihoji makumi ya mabilioni ya dola zilizotumiwa na Washington kwa Ukraine -- zaidi ya dola bilioni 60 kama msaada wa kijeshi tangu mashamulizi ya Urusi mnamo Februari 2022.
Kwa hivyo Rais anayemaliza muda wake Joe Biden anataka kuharakisha utoaji wa misaada ya kijeshi kwa Ukraine na kuendelea kuweka utaratibu ili nchi za Ulaya zichukue nafasi hiyo.
Kuna mabaki ya bahasha iliyopigiwa kura katika msimu wa kuchipua hadi dola bilioni 9.2 kutengwa, ikijumuisha bilioni 7.1 kuchukua kutoka kwa hisa za Marekani na bilioni 2.1 kufadhili kandarasi za ununuzi wa silaha, kulingana na Pentagon.
Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa White House Jake Sullivan aliongeza kiasi cha dola bilioni sita siku ya Jumapili na kuonya juu ya hatari ya kusitisha uungwaji mkono kutoka kwa Marekani.
"Mwisho wa utawala (unaomaliza muda wake), watajaribu kusafirisha chochote kinachopatikana," kama vile magari ya kivita na risasi za silaha ndogo ndogo, "ambavyo Ukraine inahitaji na ambavyo Marekani ina kiasi kikubwa," Mark. Cancian wa Kituo cha Mafunzo ya Kimataifa na Kimkakati (CSIS) huko Washington ameliambia shirika la habari la AFP.
- Nchi za Ulaya chini ya shinikizo -
Wakati Berlin ikiwa katika mzozo wa kisiasa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ameonya juu ya hatari ya kuona Vladimir Putin akitumia fursa ya mabadiliko ya kisiasa nchini Marekani kushinikiza faida yake nchini Ukraine.
Kila kitu ambacho Ulaya inaweza kuleta Ukraine "lazima kihamasishwe sasa", amesema waziri huyo, akisisitiza kuimarisha ulinzi wa anga wa nchi hiyo.
Comments
Post a Comment