Chad yatangaza kuvunja makubaliano yake ya ushirikiano wa kiulinzi na Ufaransa

 

Chad yatangaza kuvunja makubaliano yake ya ushirikiano wa kiulinzi na Ufaransa

Saa chache baada ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noël Barrot nchini Chad, waziri mwenzake Abderaman Koulamallah amechapisha taarifa kwa vyombo vya habari hivi punde siku ya Alhamisi, Novemba 28 kubaini"mwisho wa ushirikiano wa kiulinzi uliotiwa saini na Jamhuri ya Ufaransa".

Askari wa Ufaransa akilinda lango la kambi ya kikosi cha jeshi la anga inayoitwa kambi ya anga 172 "Sergent-chef Adji Kossei", huko N'Djamena, Chad, Mei 14, 2024.
Askari wa Ufaransa akilinda lango la kambi ya kikosi cha jeshi la anga inayoitwa kambi ya anga 172 "Sergent-chef Adji Kossei", huko N'Djamena, Chad, Mei 14, 2024. © Joris Bolomey / AFP
Matangazo ya kibiashara

Chad inasitisha mkataba wa ushirikiano wa kiulinzi uliotiwa saini na Ufaransa, na kurekebishwa mwaka wa 2019. Bila, kwa sasa, kutoa maelezo zaidi kuhusu kusitishwa kwa mkataba huu. Tangazo hilo limetolewa sio wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noël Barrot ya saa 24 nchini humo, lakini saa chache baada ya kuondoka kwake.

"Serikali ya Jamhuri ya Chad inafahamisha raia wake na jumuiya ya kimataifa kuhusu uamuzi wake wa kusitisha mkataba wa ushirikiano wa kiulinzi uliotiwa saini na Jamhuri ya Ufaransa," amesema Abderaman Koulamallah katika taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Facebook ya wizara hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad anabaini kwamba Chad inataka kubadilika, lakini Ufaransa inasalia kuwa mshirika muhimu. N'Djamena inahakikisha kwamba masharti yaliyotolewa kwa ajili ya kusitishwa kwa mkataba huo, ikiwa ni pamoja na muda wa notisi, yataheshimiwa. "Serikali inapenda kusisitiza kwamba uamuzi huu hautii shaka uhusiano wa kihistoria na uhusiano wa urafiki kati ya mataifa hayo mawili," inaongeza taarifa kwa vyombo vya habari kutoka wizara hiyo, ambayo inatarajia "mabadiliko ya usawa" na bado iko "wazi" kwa mazungumzo yenye kujenga ili kuchunguza aina mpya za ushirikiano”.

Taarifa kamili kwa vyombo vya habari kutoka kwa msemaji wa serikali na Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Tchad Diplomatie Alhamisi hii, Novemba 28, 2024
Taarifa kamili kwa vyombo vya habari kutoka kwa msemaji wa serikali na Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Tchad Diplomatie Alhamisi hii, Novemba 28, 2024 © Gouvernement du Tchad

Je, kauli hii ina maana gani? Je, huku ni kuondoka kwa wanajeshi wote wa Ufaransa kutoka ardhi ya Chad? Kuna karibu wanajeshi 1,000, anakumbusha mwandishi wetu wa habari Alexandra Brangeon. Je, huu ni wito wa kutazama upya ushirikiano? Maswali ambayo hayajajibiwa kwa sasa: hakuna kilichofichuliwa kufuatia mahojiano siku hiyo hiyo kati ya Rais wa Chad Mahamat Idriss Déby na mkuu wa diplomasia ya Ufaransa Jean-Noël Barrot. Hakuna upande ulioonekana kuonyesha dalili zozote za kuzorota kwa mahusiano. Kwa upande wa Ufaransa, hakukuwa na tamko lolote siku ya Alhamisi jioni.

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan