China yazindua hatua mpya kuimarisha biashara ya nje

 

China yazindua hatua mpya kuimarisha biashara ya nje

Saa 15 zilizopita

China imetangaza hatua mpya zinazolenga kuimarisha biashara ya kigeni, huku Beijing ikipambana kuboresha uchumi wake unaozidi kutishiwa na sera zinazotarajiwa kuwa za uhasama za Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump.

https://p.dw.com/p/4nG9x
Nakili kiunganishi
Xi Jinping akiwa  Lima
Rais wa China Xi JinpingPicha: Fernando Vergara/AP Photo/picture alliance

China imetangaza hatua mpya zinazolenga kuimarisha biashara ya kigeni, huku Beijing ikipambana kuboresha uchumi wake unaozidi kutishiwa na sera zinazotarajiwa kuwa za uhasama za Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump.

Uchumi huo wa pili kwa ukubwa duniani umekuwa ukipambana kufufuka tangu mlipuko wa janga la UVIKO-19, na unaendelea kuathiriwa na na mzozo wa madeni katika sekta muhimu ya nyumba, viwango duni vya ununuzi na ukosefu mkubwa wa ajira kwa vijana. Rais Xi aongeza juhudi za kuinadi China kama kinara wa utandawazi

Hali imezidi kuwa ya mashaka kufuatia kuchaguliwa tena kwa Trump, ambaye katika muhula wake wa kwanza alipandisha pakubwa ushuru kwa bidhaa za China na kusababisha vita vya kibiashara.

Wizara ya Biashara ya China imetoa agizo kwa ngazi zote za serikali kutekeleza haraka sera tisa za kukuza biashara ya kigeni, ikiwemo kupanua bima ya mikopo ya mauzo ya nje, msaada wa kifedha kwa kampuni za kigeni, na kuboresha utatuzi wa masuala ya biashara ya mipakani.

Hatua nyingine ni kukuza biashara ya mtandao ya kuvuka mipaka, kusukuma mauzo ya bidhaa maalum za kilimo na kutoa msaada kwa uagizaji wa vifaa muhimu na nishati.

 

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan