COP29: Nchi za visiwa vidogo zashutumu 'dharau' kwa rasimu ya makubaliano

 

COP29: Nchi za visiwa vidogo zashutumu 'dharau' kwa rasimu ya makubaliano

Muungano wa nchi za visiwa vidogo (Aosis) umeshutumu siku ya Ijumaa Novemba 22 "dharau" kwa "watu walio katika mazingira magumu", baada ya kuchapishwa kwa rasimu ya makubaliano katika mkutano wa 29 wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi (COP29) inayotoa dola bilioni 250 kila mwaka katika ufadhili wa hali ya hewa kutoka nchi tajiri.

Mukhtar Babayev, Rais wa COP29 akizungumza katika kikao wakati wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Hewa (COP29), Ijumaa, Novemba 22, 2024, mjini Baku, Azerbaijan.
Mukhtar Babayev, Rais wa COP29 akizungumza katika kikao wakati wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Hewa (COP29), Ijumaa, Novemba 22, 2024, mjini Baku, Azerbaijan. © AP - Peter Dejong
Matangazo ya kibiashara

“Tunasihi dhamiri ya kiadili ya wale wanaodai kuwa washirika wetu ili wawe upande wetu, wanyooshe mkono wao kwetu na wasituache,” lashutumu kundi hili la visiwa katika Pasifiki, Karibea au kutoka Afrika.

Katika COP29, toleo la makubaliano ya mwisho halikumridhisha yeyote... na hasa nchi za Kusini. Hawawezi “kubaki mateka wa biashara [hizi] za kisiasa,” amesema waziri wa Colombia.

Nchi tajiri hatimaye zimeweka kadi zao katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa hali ya hewa mjini Baku kwa kupendekeza dola bilioni 250 kwa mwaka kwa ajili ya hatua za hali ya hewa. Pendekezo "halikubaliki kabisa", rais wa kundi la Afrika amejibu siku ya Ijumaa katika mkutano wa 29 wa Umoja wa Mataifa kuhusu tabianchi (COP29) huko Baku.

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan