Côte d'Ivoire: Watu 20 wafariki baada ya magari mawili madogo kugongana
Côte d'Ivoire: Watu 20 wafariki baada ya magari mawili madogo kugongana
Watu 20 wamefariki Jumapili jioni katika ajali ya magari mawili madogo yaliyogongana katikati mwa Côte d'Ivoire, kwa mujibu wa huduma za ulinzi wa raia (ONPC).
Imechapishwa: Imehaririwa:
"Mabasi mawili madogo yanayobeba watu 24 kila moja, yamegongana huko Ahizabré, kijiji kilichoko takriban kilomita 20 kutoka Gagnoa, kwenye barabara inayotoka Gagnoa kuelekea Soubré. Ripoti ya muda inaonyesha kuwa watu 31 wamejeruhiwa na vifo 20 vilivyothibitishwa na muuguzi katika kituo cha afya cha kijiji hicho", ONPC inabainisha kwenye wake wa Facebook. Kwa mujibu wa ONPC, ajali hiyo ilitokea majira ya saa 1:30 usiku na shughuli ya uokoaji ya wazima moto wa mkoa huo "imekamilika".
Kama ilivyo katika nchi nyingi za Kiafrika, ajali mbaya hutokea mara kwa mara nchini Côte d'Ivoire kutokana na ubovu wa baadhi ya barabara na magari mengi, pamoja na utovu wa nidhamu wa madereva. Madereva wengi pia wanamiliki leseni walizonunua bila kuwahi kupitia shule ya udereva.
Mnamo mwezi wa Septemba, watu 13 waliteketea kwa moto katika ajali mbaya, baada ya basi kugongana na lori la mafuta kaskazini mwa nchi. Kati ya watu 1,000 na 1,500 wanauawa kwa wastani kila mwaka katika ajali za barabarani nchini Côte d'Ivoire, kulingana na Wizara ya Uchukuzi, kwa magari milioni 1.5 yanayofanya kazi nchini humo. Kwa kulinganisha, Ufaransa - ambayo sio mwanafunzi bora zaidi barani Ulaya - inarekodi vifo 3,500 kwa magari milioni 39 kwa wastani.
Katika miaka ya hivi karibuni, Côte d'Ivoire imechukua mfululizo wa hatua za kupunguza ajali mbaya: vibali vya pointi, marufuku ya kuagiza magari yenye zaidi ya umri wa miaka mitano, ufuatiliaji wa video na ukarabati wa barabara hasa. Côte d'Ivoire inatarajia kupunguza idadi ya vifo katika barabara zake kwa 50% ifikapo mwaka 2025.
Comments
Post a Comment