Greenpeace yachukizwa na makubaliano ya COP29

 

Greenpeace yachukizwa na makubaliano ya COP29

Saleh Mwanamilongo
Saa 5 zilizopita

Shirika la kimataifa la Mazingira la Greenpeace limekosoa makubaliano yaliyofikiwa mapema leo katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29.

https://p.dw.com/p/4nMqt
Nakili kiunganishi
Shirika la kimataifa la Mazingira la Greenpeace lakosoa makubaliano ya Baku kwenye mkutano wa Mabadaliko ya tabia nchi
Shirika la kimataifa la Mazingira la Greenpeace lakosoa makubaliano ya Baku kwenye mkutano wa Mabadaliko ya tabia nchiPicha: Simon Shin/Zumapress/picture alliance

Jasper Inventor, mkuu wa ujumbe wa shirika la Greenpeace kwenye mazungumzo ya COP29 amesema watu wamechoshwa na wamekata tamaa. Inventor amesema ahadi ya mataifa tajiri kutoa dola bilioni 300 kwa nchi masikini haitoshi kwa mahitaji yao. Na kuongeza kuwa shirika la Greenpeace na wengine wanasubiri mkutano ujao wa COP30, huko Brazil, kurekebisha makubaliano yaliofikiwa sasa.

Nchi zinazoendelea na wanaharakati wengi hawakuridhishwa na makubalano yaliofikiwa leo huko Baku.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, nchi tajiri zitatoa ufadhili wa dola bilioni 300 kwa mwaka, katika kipindi cha miaka kumi, kwa nchi masikini ilikupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan