Hezbollah yakataa usitishaji vita wowote na Israel ambao utakiuka 'uhuru' wa Lebanoni
Hezbollah yakataa usitishaji vita wowote na Israel ambao utakiuka 'uhuru' wa Lebanoni
Kiongozi mpya wa Hezbollah, Sheikh Naïm Qassem, amebainisha siku ya Jumatano Novemba 20 kwamba hakuna makubaliano ya kusitisha mapigano yatakubaliwa ikiwa yatakiuka "uhuru" wa Lebanoni. Hii ni kujibu nia ya Israel ya kutaka "uhuru wa kuchukua hatua" katika ardhi ya Lebanoni dhidi ya kundi la Kishia, endapo kutakuwa na makubaliano.
Imechapishwa:
Kiongozi wa Hezbollah ametoa idhni kutafuta suluhu la kidiplomasia kwa vita vinavyoendelea na Israel. Hata hivyo, alionya kuwa hataachana na chaguo la kijeshi kukabiliana na majaribio ya Israel ya kukalia kwa mabavu ardhi ya Lebanoni. Kwenye mahojiano na televisheni, Naïm Qassem ametangaza kwamba Israel "haiwezi kuweka masharti yake" kwa Hezbollah, wakati Washington ilituma mjumbe wake maalum kunyamanzisha silaha.
Sheikh Naïm Qassem ameonyesha uungwaji wake mkono kwa Spika wa Bunge, Nabih Berri. Kiongozi mkuu wa Kishia katika serikali, Nabih Berri, alipewa mamlaka ya kufanya mazungumzo kwa niaba ya Hezbollah na mjumbe maalum wa Joe Biden, Amos Hochstein. Amos Hochstein alifanya siku mbili huko Beirut kabla ya kuondoka kwenda Tel Aviv siku ya Jumatano jioni, pamoja na majibu ya Lebanoni kwa makubaliano yaliyopendekezwa kati ya Lebanoni na Israeli.
Pendekezo ambalo litafikia "kusitishwa kabisa kwa mapigano, huku uhuru wa Lebanoni ukiheshimiwa", amebainisha Naïm Qassem, ambaye amekataa kutoa maelezo ya makubaliano yanayoendelea.
Comments
Post a Comment