Jopo la WHO lasema mpox bado ni kitisho cha afya duniani

 

Jopo la WHO lasema mpox bado ni kitisho cha afya duniani

Saa 3 zilizopita

Shirika la Afya Ulimwenguni - WHO limesema kuwa mlipuko wa mpox unaendelea kuwa dharura ya afya ya umma duniani. Kamati inayowajumuisha watalaamu huru ilifanya uamuzi huo kwenye mkutano jijini Geneva.

https://p.dw.com/p/4nLK8
Nakili kiunganishi
Utoaji chanjo ya mpox nchini Kongo
WHO ilitangaza mwezi Agosti dharura ya afya kutokana na kusambaa kwa mpoxPicha: Ernest Muhero/DW

Ulijiri miezi mitatu baada ya WHO mwezi Agosti kutangaza dharura ya afya kutokana na kusambaa kwa mpox, ikifahamika awali kama homa ya nyani, barani Afrika.

Soma pia:Kongo yakabiliwa na uhaba wa chanjo ya Mpox

Aina mpya ya kirusi cha ugonjwa huo, inayofahamika kama Clade 1b, ambacho kilisambaa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inazusha hofu ya kusababisha magonjwa mengine makali zaidi.

Kwa mujibu wa WHO, zaidi ya visa 50,000 vinavyoshukiwa kuwa vya mpox viliripotiwa kwenye nchi za Kiafrika mwaka huu. Kulikuwa na zaidi ya vifo vya watu 1,080. Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa barani Ulaya kinakadiria hatari ya mpox kwa umma barani Ulaya kuwa ndogo.

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan