Kombora la Israel laua mkurugenzi wa hospital Lebanon

 

Kombora la Israel laua mkurugenzi wa hospital Lebanon

Saa 17 zilizopita

Wizara ya Afya ya Lebanon imesema mkurugenzi wa hospitali moja ameuawa kwenye mashambulizi ya anga ya Israel. Mkurugenzi huyo ameuawa akiwa nyumbani kwake kaskazini mashariki mwa Lebanon.

https://p.dw.com/p/4nLU6
Nakili kiunganishi
Libanon I Beirut -  Israelischer Luftangriff
Wafanyakazi wa uokoaji na watu wanatafuta waathirika wa shambulio la anga la Israeli huko Beirut, Lebanon, mapema Jumamosi, Novemba 23, 2024.Picha: Bilal Hussein/AP/picture alliance

Watu wengine sita waliuawa kwenye shambulizi hilo. Wakati huo huo shambulizi kama hilo kwenye upande wa kusini mwa taifa hilo limesababisha vifo vya wahudumu watano wa afya. Katika eneo la Gaza mkurugenzi wa hospitali ya Kamal Adwan, kituo cha afya kati ya vichache vyenye kutoa huduma kidogo huko kaskazini mwa ukanda wa Gaza amesema Israel imekishambulia kituo hicho kwa makombora, wafanyakazi 9 wamejeruhiwa na mifumo mingine ya nishati na tiba imeharibiwa. Hata hivyo jeshi la Israel limesema halijui chochote kuhusu mashambulizi katika eneo hilo. Vita kamili kati ya Israel na Hezbollah vilizuka mwezi Septemba baada ya takriban mwaka mmoja wa mzozo. Zaidi ya watu 3,640 wameuawa na wengine 15,350 wamejeruhiwa nchini humo.

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan