Marekani yaahidi kuendeleza juhudi, kuzuia ongezeko la joto

 

Marekani yaahidi kuendeleza juhudi, kuzuia ongezeko la joto

Saa 7 zilizopita

Mjumbe wa ngazi za juu wa masuala ya mazingira wa nchini Marekani ameyahakikishia mataifa kwamba taifa hilo halitabadilisha msimamo wake hata baada ya kurejea kwa Donald Trump madarakani.

https://p.dw.com/p/4mtl1
Nakili kiunganishi
Baku COP29-Logo
Mkutano wa kilele wa kimataifa wa masuala ya mazingira COP29 unafanyika Baku, AzerbaijanPicha: Jakub Porzycki/NurPhoto/picture alliance

Mjumbe wa ngazi za juu wa masuala ya mazingira wa nchini Marekani ameyahakikishia mataifa yanashiriki mkutano wa kimataifa wa mazingira wa COP29 kwamba kurejea kwa rais mteule Donald Trump hakutahitimisha juhudi za taifa hilo za kudhibiti ongezeko la joto duniani.

Mjumbe wa Marekani John Podesta amekiri kwamba utawala ujao wa Marekani utajaribu kubadilisha mkondo, lakini amesema Wamarekani wenyewe watajua namna ya kuikabili hali hiyo.

Licha ya vita nikuvute ya jana Jumatatu baada ya mazungumzo hayo kufunguliwa mjini Baku, serikali ziliidhinisha viwango vipya vya Umoja wa Mataifa vya uzalishaji wa gesi ya kaboni.

Rais wa COP29 Mukhtar Babayev amesifu hatua hiyo iliyofikiwa baada ya miaka kadhaa ya majadiliano magumu.

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan