Mkuu wa IAEA akaribisha uamuzi wa Iran kuhusu mpango nyuklia

 

Mkuu wa IAEA akaribisha uamuzi wa Iran kuhusu mpango nyuklia

Saa 3 zilizopita

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki IAEA, Rafael Grossi amesema Iran imekubali ombi la kuzingatia kurutubisha hadi asilimia 60 ya madini ya Urani na kutovuka kiwango hicho.

https://p.dw.com/p/4nEB3
Nakili kiunganishi
Mkuu wa IAEA Rafel Grossi
Rafael Grossi amesema Iran imekubali ombi la kuzingatia kurutubisha hadi asilimia 60 ya madini ya UraniPicha: Askin Kiyagan/Anadolu/picture alliance

Matamshi hayo aliyatoa katika mkutano wa IAEA mjini Vienna, Austria, huku mataifa yenye nguvu ya Ulaya na Marekani yakiwasilisha azimio la kuikemea Iran kwa ushirikiano wake mbaya na IAEA.

Soma pia:Iran yaonya azimio la nchi tatu za Ulaya ndani ya IAEA litavuruga mambo 

Akizungumza na waandishi habari, Grossi alikaribisha kile alichokiita "hatua thabiti” ya Iran kukubali kuweka ukomo kwenye mpango wake wa urutubishaji madini ya urani.

Na kufuatia ripoti za uharibifu kwenye mpango wa nyuklia wa Iran uliosababishwa na shambulizi la Israel, Grossi ametoa wito wa sheria ya kimataifa kuheshimiwa. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliliambia bunge la Israel Jumatatu wiki hii kuwa sehemu ya mpango wa nyuklia wa Iran iliharibiwa katika shambulizi la kijeshi la Israel mwezi Oktoba.

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan