Rais wa Uganda awasamehe viongozi 19 wa upinzani
Rais wa Uganda awasamehe viongozi 19 wa upinzani
Rais wa Uganda amewasamehe viongozi 19 wa upinzani siku ya Ijumaa, kufuatia kutiwa hatiani na mahakama ya kijeshi kwa "uhaini" na "kumiliki silaha kinyume cha sheria." Vyama vya upinzani vimekandamizwa chini ya utawala wa rais Yoweri Museveni, ambaye ameongoza nchi hiyo tangu mwaka 1986.
Imechapishwa:
"Ninatoa msamaha kwa wale waliopatikana na hatia ya uhaini (...) na kumiliki silaha kinyume cha sheria," Bw. Museveni amesema. Viongozi 16 wa chama cha upinzani cha NUP (National Unity Platform) walihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela mwezi Oktoba na mahakama ya kijeshi kwa "uhaini na kumiliki vilipuzi kinyume cha sheria". Viongozi wengine watatu wa NUP walipatikana na hatia kwa mashtaka kama hayo.
Mnamo mwezi wa Oktoba, mahakama iliamua kwamba hukumu iliyotolewa ingepunguzwa hadi miezi mitatu na siku 22 gerezani, kutokana na miaka ambayo tayari imepita wakiwa katika kizuizini cha kabla ya kesi. Wakili Shamim Malende, mwanasheria wa chama hicho, alielezea shutuma hizo kama "za kutia shaka".
Wote walikiri mashtaka lakini kiongozi wa NUP Bobi Wine - ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi - anasema walilazimishwa kufanya hivyo na kuomba msamaha wa rais. Mamlaka za Uganda mara kwa mara hunyooshewa kidole cha lawama na mashirika ya haki za binadamu.
Mnamo mwaka 2021, wakati wa uchaguzi uliopita wa urais, uligubikwa na udanganyifu kulingana na upinzani, maandamano ya kupinga kukamatwa tena kwa Bobi Wine yalikandamizwa kwa nguvu na polisi, na kusababisha vifo vya takriban watu 54.
Comments
Post a Comment