Saudi Arabia: Viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu walaani 'mauaji ya kimbari' yanayoendelea Gaza
Saudi Arabia: Viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu walaani 'mauaji ya kimbari' yanayoendelea Gaza
Riyadh imezialika nchi 22 za Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na madola hamsini yaliyokusanyika ndani ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu siku ya Jumatatu Novemba 11, 2024. Mkutano unaohusu migogoro inayoendelea katika eneo hilo ambao pia atakabiliana nao Donald Trump ambaye anajiandaa kurejea White House.
Imechapishwa:
Katika ufunguzi wa mkutano wa kilele unaohusu vita vya Israel katika Ukanda wa Gaza na Lebanoni, Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman ametumia neno "mauaji ya halaiki" kuelezea operesheni za kijeshi za Israel katika Ukanda wa Gaza. “Tunatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua majukumu yake [...] kwa kukomesha mara moja mashambulizi ya Israel dhidi ya ndugu zetu huko Palestina na Lebanoni. "
Viongozi wa nci za Kiarabu na Kiislamu waliokusanyika huko Riyadh walichukua msimamo sawa dhidi ya Israeli, wakilaani "mauaji ya halaiki" na "uhalifu wa kutisha na wa kuhuzunisha" wa jeshi la Israeli huko Gaza, "haswa kaskazini mwa Ukanda". Wamelaani mateso, mauaji, visa vya watu kutoweka na "kutaka kuangamiza kabila," kulingana na taarifa ya mwisho ya mkutano huo.
Mohammed bin Salman, mwenyeji wa mkutano wa Riyadh, pia ametoa wito kwa Israel "kuheshimu mamlaka ya ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran" na "kujizuia kushambulia ardhi yake". Wanachama wengi wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu watakubaliana na matamko haya madhubuti. Hata kama kuna tofauti kubwa kati ya nchi ambazo zimerekebisha uhusiano wao na Israeli na zile zinazoipinga, kuanzia na Jamhuri ya Kiislamu.
"Jamhuri ya Dada"
Mrithi wa kiti cha enzi, kiongozi mkuu wa Saudi Arabia, pia ameielezea Iran kama "jamhuri dada", ishara ya kuongezeka kwa uhusiano kati ya madola mawili ya Mashariki ya Kati, ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakiunga mkono kambi zinazopingana katika eneo hilo, haswa katika nchini Syria na Yemen.
Iran, nchi yenye Washia wengi, na Saudi Arabia, utawala wa kifalme wa Kisunni, zilirejesha uhusiano wa kidiplomasia mwezi Machi 2023 baada ya miaka saba ya mvutano, kama sehemu ya makubaliano yaliyojadiliwa chini ya uangalizi wa China. Nchi hizo mbili zimeongeza mawasiliano tangu kuzuka kwa vita huko Gaza mnamo mwezi Oktoba 2023, baada ya shambulio la Hamas huko Israeli mnamo Oktoba 7. Iran inaunga mkono vuguvugu la Waislam wa Palestina huku Saudi Arabia ikitaka kudhibiti upanuzi wa mzozo huo.
Katika mkutano huu wa kilele wa nchi za Kiarabu na Kiislamu, makamu wa kwanza wa rais wa Iran, Mohammad Reza Aref, ameelezea mauaji ya viongozi wa Hamas ya Palestina na Hizbollah ya Lebanoni yaliyofanywa na Israel kama "ugaidi uliopangwa." "Operesheni zinazoelezewa kama "mauaji yaliyolengwa," ambapo wasomi wa Kipalestina na viongozi wa nchi zingine katika eneo hilo wanauawa mmoja baada ya mwingine au kwa wingi, si chochote isipokuwa ugaidi uliopangwa," amesema.
Wakati wa hotuba yake siku ya Jumatatu, Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati amebainisha kwamba mgogoro "usio na kifani" unatishia kuwepo kwa nchi yake. Pia ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa "kuendelea kutuma msaada kwa Lebanoni" na kutoa wito wa kukomesha uingiliaji wowote "katika masuala yake ya ndani". Mwishoni mwa mwezi wa Oktoba, Najib Mikati alikosoa kwa mara ya kwanza "uingiliaji wa wazi wa Iran", shutuma zilizopingwa na Tehran.
Comments
Post a Comment