Senegal: Machafuko ya kisiasa yaripotiwa kuelekea uchaguzi wa wabunge

 

Senegal: Machafuko ya kisiasa yaripotiwa kuelekea uchaguzi wa wabunge

Nchini Senegal, kuelekea uchaguzi wa wabunge siku ya Jumapili, muungano wa mashirika 46 ya kiraia unaonya kuwepo kwa ongezeko la machafuko ya kisiasa katika kipindi hiki cha kampeni.

Rais wa  Senegal Basirou Diomaye Faye.
Rais wa Senegal Basirou Diomaye Faye. REUTERS - Abdou Karim Ndoye
Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya kiraia yanayofuatilia mwenendo wa kampeni hizo katika maeneo mbalimbali ya nchi, yanasema kuna matumizi makubwa ya rasilimali za umma kama maafisa wa usalama, kuwahangaisha wanasiasa wa upinzani wanapoendelea kuomba kura.

Aidha, Mashirika hayo yametoa mfano wa Waziri wa afya aliyeamua kupelekea vifaa vya kutoa tiba katika eneo la Podor Kaskazini mwa nchi hiyo, kuwashawishi wapiga kura kumuunga mkono, kitendo ambacho kimetajwa ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma kufanya kampeni.

Asilimia 26 ya vitendo hivi vilishuhudiwa ndani ya siku 10 ya kampeni, huku asilimia 20 ya vitendo vya rushwa vikiripotiwa kwa waangalizi hao.

Ofisi za vyama vya upinzani, zimeteketezwa moto jijini Dakar huku vipeperushi na mabango ya wagombea hao yakiharibiwa.

Licha ya changamoto hizi, waangalizi wa uchaguzi huo kutoka mashirika ya kiraia wanasema wameridhika namna Tume ya uchaguzi ilivyojiandaa kusimamia uchaguzi huo.

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan