Serikali ya Mali yafunga kituo cha televisheni cha kibinafsi

Serikali ya Mali yafunga kituo cha televisheni cha kibinafsi Sudi Mnette Saa 14 zilizopitaSaa 14 zilizopita Mamlaka ya Kijeshi ya Mali imekifunga kituo cha utangazaji cha kibinafsi baada ya mshirika wake mwenza ambayo pia inaendeshwa kijeshi Burkina Faso kulalamikia utangazaji wake. https://p.dw.com/p/4nLjS Nakili kiunganishi Russland Mali Militärjunta untersagt politische Aktivitäten | Assimi Goita Rais wa Mali Assimi Goita akihudhuria mkutano wa kilele wa Urusi na Afrika huko Saint Petersburg, Urusi, Julai 29, 2023. Picha: Alexander Ryumin/TASS Host Photo Agency via REUTERS Matangazo Afisa mmoja wa kituo hicho aliyezungumza kwa msaharti ya kutotajwa jina lake aliliambia shrika la habari la AFP kwamba mamlaka ya mawasiliano ya Mali ilizuia leseni ya Joliba TV News kuanzia tarehe 26 Novemba. Hatua hiyo inafuatia malalamiko yaliyowasilishwa dhidi ya kituo hicho Novemba 12 na mamlaka ya mawasiliano ya Burkina Faso kuhusu maoni yaliyotolewa na mwanasiasa wa Mali Issa Kaou N'Djim kuhusu serikali ya Burkina Faso yenyewe. Anatarajiwa kushtakiwa kwa kumkashifu hadharani mkuu wa nchi ya kigeni Desemba 23. Mataifa hayo mawili ya Afrika Magharibi yanatawaliwa na tawala za kijeshi tangu mapinduzi ya mwaka 2020 na 2022, yakiungana na Niger inayoongozwa pia kijeshi ambayo yameunda shirikisho la Muungano wa Nchi za Sahel (AES).

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan