Sudan: Baraza la usalama la UN kuchukua hatua dhidi ya pande hasimu
Sudan: Baraza la usalama la UN kuchukua hatua dhidi ya pande hasimu
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanathathmini azimio lililoandaliwa na Uingereza, kutaka jeshi na wanamgambo wa RSF nchini Sudan, kusitisha mapigano na kuruhusu misaada ya kibindamu kuwafikia mamilioni ya watu walioathiriwa na mzozo huo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Azimio hilo linahitaji kuungwa mkono kwa kura tisa bila ya kuwepo kwa kura ya turufu kutoka wajumbe wakudumu ambao ni kutoka Marekani, Ufaransa, Uingereza, Urusi na China. Uingereza inataka azimio hilo kupigiwa kura haraka iwezekanvyo.
Itakumbukwa kuwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha maazimio mawili ya awali kuhusu Sudan mwezi Machi na kutoa wito wa kusitishwa mara moja kwa uhasama wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Haya yanajiri wakati huu, ikiwa ni mara ya kwanza kwa wataalam wa Umoja wa Mataifa kuzuru mji wa Port Sudan, kwa siku tatu, kujionea hali ilivyo hasa kwenye jimbo la Darfur.
Umoja wa Mataifa umesema karibu watu milioni 25, nusu ya wakazi wa Sudan wanahitaji msaada huku njaa ikishuhudiwa katika kambi za wakimbizi na watu milioni 11 wamekimbia makazi yao. Karibu milioni 3 ya watu hao wamekwenda nchi zingine kuwa wakimbizi.
Comments
Post a Comment