Sudan Kusini: Milio ya risasi yasikika katika mji mkuu wa Juba

 

Sudan Kusini: Milio ya risasi yasikika katika mji mkuu wa Juba

Nchini Sudan Kusini, milio ya risasi iliskika siku ya Alhamis katika mji mkuu, Juba, nyumbani kwa mkuu wa upelelezi aliyefutwa kazi hivi majuzi, Akol Koor, huku Umoja wa Mataifa ukitaja tukio hilo kama jaribio la kukamatwa kwa afisa huyo.

Rais Salva Kiir alimfuta kazi Akol Koor aliyekuwa kiongozi wa idara ya upelelezi.
Rais Salva Kiir alimfuta kazi Akol Koor aliyekuwa kiongozi wa idara ya upelelezi. © Tony Karumba / AFP
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano hayo baina ya wanajeshi wa serikali na maafisa wanaomlinda Akol Koor, yalidumu kwa takriban saa moja na kusababisha makumi ya maafisa wake kuuawa au kujeruhiwa.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa Koor aliyefutwa kazi na Rais Salva Kiir mwezi Oktoba alikamatwa wakati wa makabiliano hayo lakini taarifa hizo hazijadhibitishwa na mamlaka.

Akol amekuwa chini ya kifungo cha nyumbani tangu atimuliwe kazi, lakini alisalia kuwa mtu mwenye nguvu baada ya kuongoza idara ya Usalama wa Taifa tangu taifa hilo kupata uhuru mwaka 2011.

Akithibitisha ufyatulianaji huo wa risasi, msemaji wa jeshi nchini humo alisema wanajeshi walitumwa huko ili kutoa usalama zaidi kabla ya mapigano hayo kuzuka.

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan