Sudan: Watu zaidi ya 40 wameuawa katika mashambulio ya wapiganaji wa RSF

 

Sudan: Watu zaidi ya 40 wameuawa katika mashambulio ya wapiganaji wa RSF

Mashambulio ya wapiganaji wa RSF yaliyoanza Jumanne wa wiki hii kwenye jimbo la Al Jazira nchini Sudan, yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 40 na wengine mamia kujeruhiwa, ripoti za mashirika ya misaada zimeonesha.

Jimbo la Al Jazira  kwa miezi kadhaa limekuwa kitovu cha mapigano kati ya wanajeshi wa Serikali na kundi la RSF linalowania umiliki wa eneo hilo.
Jimbo la Al Jazira kwa miezi kadhaa limekuwa kitovu cha mapigano kati ya wanajeshi wa Serikali na kundi la RSF linalowania umiliki wa eneo hilo. REUTERS - Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa madaktari katika kituo cha afya cha Wad Rawah kwenye jimbo hilo, wanasema wagonjwa wengi waliowapokea walikuwa na mejeraha ya risasi, kituo hiki kikishambuliwa mara kadhaa na wapiganaji hao.

Aidha baadhi ya mashuhuda wa mashambulio hayo, wameliambia shirika la habari la AFP kuwa, wapiganaji hao ambao wamekuwa vitani na jeshi la Serikali tangu mwezi April mwaka uliopita, walianza kwa kushambulio kijiji kilichoko umbali wa kilometa 100 na jimbo la Al Jazira.

Pande hasimu nchini Sudan zimekuwa zikipambana kudhibiti maeneo mbalimbali muhimu kwenye taifa hilo.
Pande hasimu nchini Sudan zimekuwa zikipambana kudhibiti maeneo mbalimbali muhimu kwenye taifa hilo. REUTERS - Staff

Jimbo hili kwa miezi kadhaa limekuwa kitovu cha mapigano kati ya wanajeshi wa Serikali na kundi la RSF linalowania umiliki wa eneo hilo.

Haya yanajiri wakati huu Marekani na washirika wake wakiendelea kuvutana kuhusu namna ya kutatua mzozo wa Sudan, wakati huu pia maelfu ya raia wakiendeleea kuuawa na wengine mamilioni wanaendelea kuwa wakimbizi.

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan