Tanzania: Chama tawala chashinda 98% ya viti katika chaguzi za mitaa, waziri atangaza

 

Tanzania: Chama tawala chashinda 98% ya viti katika chaguzi za mitaa, waziri atangaza

Chama tawala nchini Tanzania, Chama Cha Mapinduzi, ambacho kimetawala siasa kwa miongo kadhaa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, kimeshinda zaidi ya asilimia 98 ya viti katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika wiki hii, Waziri wa Nchi ametangaza siku ya Alhamisi jioni Novemba 28.

Wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakifanya mkutano wao wa mwisho wa kampeni kabla ya uchaguzi. Chama hicho kiko madarakani tangu mwaka 1961.
Wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakifanya mkutano wao wa mwisho wa kampeni kabla ya uchaguzi. Chama hicho kiko madarakani tangu mwaka 1961. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Viongozi hawa waliochaguliwa wanapaswa kula kiapo mara moja na kuanza kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi katika majimbo yao," amesema Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Nchi anayesimamia uchaguzi katika ofisi ya Rais.

Uchaguzi huu, unaochukuliwa na waangalizi wengi kama kipimo wa kidemokrasia katika mazingira ya kuongezeka kwa ukandamizaji wa kisiasa katika miezi ya hivi karibuni katika nchi hii ya Afrika Mashariki - ambayo itafanya uchaguzi wake wa urais na wabunge mwaka ujao - ulizua shutuma za udanganyifu pamoja na ghasia.

Chama kikuu cha upinzani, Chadema, kililaani mauaji ya wanachama wake watatu kati ya Jumanne jioni na Jumatano, katika matukio yanayohusiana na upigaji kura.

Takriban wapiga kura milioni 31 waliitwa kwenye uchaguzi ili kuwateua zaidi ya viongozi 80,000 kutoka miji, vijiji na vitongoji.

Huu pia ulikuwa uchaguzi wa kwanza tangu kuingia madarakani kwa Samia Suluhu Hassan, ambaye kama makamu wa rais alichukua nafasi ya John Magufuli, aliyefariki ghafla mwezi Machi 2021.

Kwa miezi kadhaa, upinzani, ambao ulisusia uchaguzi uliopita wa mwaka 2019, umelaani kukithiri kwa ukandamizaji dhidi yake.

Comments

Popular posts from this blog

Mali: Wanachama wa Azimio la Machi 31 watoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa

Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Iran yailaani Daesh (ISIS) kwa kumuua waziri wa serikali Taliban Afghanistan