Waziri Mkuu mpya wa Haiti Alix Didier Fils-Aimé aapishwa
Waziri Mkuu mpya wa Haiti Alix Didier Fils-Aimé aapishwa
Mrithi wa Gary Conille, aliyetimuliwa kwenye wadhifa wake wa waziri mkuu na Baraza la Mpito la Rais baada ya kuwa madarakani kwa miezi mitano pekee, ameapishwa hivi pune Jumatatu, Novemba 11 huko Port-au-Prince. Katika hotuba yake ya kuapishwa iliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa, Alix Didier Fils-Aimé ameahidi "kufanya kazi bila kuchoka [...] kwa uwiano wa kisiasa na "kurejesha usalama" nchini Haiti.
Imechapishwa:
Alix Didier Fils-Aimé alikuwa tayari mmoja wa waliofika fainali kwa wadhifa wa Waziri Mkuu mwezi Aprili. Baraza la Mpito la Rais hatimaye lilimaliza mzozo wake wa wazi na Garry Conille kwa kumteua kama mkuu wa serikali ya Haiti. Akiwa na umri wa miaka 52, mfanyabiashara huyo anakua waziri mkuu baada ya kuwa rais wa Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda na mgombea katika nafasi ya seneta ambaye hakufanikiwa mnamo mwaka 2016 kwa chama cha Vérite (Ukweli).
Ameapishwa Jumatatu Novemba 11 huko Port-au-Prince. Katika hotuba yake ya kuapishwa kwa Kifaransa iliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa, mkuu huyo mpya wa serikali ameahidi "kufanya kazi bila kuchoka [...] kwa uwiano wa kisiasa" na "kurejeshwa kwa usalama" nchini. "Ninajitolea [...] kuweka nguvu zangu, ustadi wangu na uzalendo wangu kwa maslahi ya kitaifa", ametangaza haswa, pia akibainisha "uchaguzi" ujao, wakati nchi ikiwa haina rais wa nchi tangu mwaka 202 .
Alix Didier Fils-Aimé anatoka katika familia ya wawekezaji huko Port-au-Prince. Baba yake anajulikana kuwa mwanaharakati kwa sababu ya kidemokrasia, alifungwa gerezani wakati wa udikteta wa Duvalier, kisha mbunge kati ya mwaka 1995 na 1999. Anajionyesha kwenye LinkedIn kama "mjasiriamali raia aliyejitolea". Mhitimu wa usimamizi wa biashara kutoka Chuo Kikuu cha Boston nchini Marekani, mkuu mpya wa serikali amefungua biashara kadhaa nchini Haiti, ikiwa ni pamoja na mnyororo wa kusafisha kavu na mtoa huduma wa mtandao wa Intanet Hainet. Alix Didier Fils-Aimé pia ni mwanachama mwanzilishi wa Chama cha Makampuni ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini Haiti (AHTIC).
Lakini Alix Didier Fils-Aimé anakabiliwa na miradi mingi. Kwanza kabisa, uteuzi wake wenyewe unapingwa na Garry Conille. Mtu huyo ambaye aliteuliwa kuwa waziri mkuu mwezi Aprili alijaribu hadi mwisho kuzuia kuchapishwa kwa jina la mrithi wake katika Jarida Rasmi: anabaini kwamba Baraza la Mpito la Rais (CPT) halina mamlaka ya kumfukuza kazi. Kwa mujibu wa Katiba, Waziri Mkuu anawajibika kwa Bunge. Lakini tangu mwezi wa Januari 2020, hakuna uchaguzi ambao umefanyika.
Ombwe hili la wabunge limesababisha mvutano wa madaraka kati ya CPT na serikali katika miezi ya hivi karibuni, pamoja na mivutano mikubwa na Garry Conille, ambayo inamsumbua mwanasheria Marie Rosy Auguste Ducéna, wa Mtandao wa Kutetea Haki za Kibinadamu nchini Haiti.
Comments
Post a Comment