Posts

Showing posts from August, 2024

Kikao cha OIC cha mjini Jeddah na majukumu ya nchi za Kiislamu

Image
  Kikao cha OIC cha mjini Jeddah na majukumu ya nchi za Kiislamu Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imeamua kuitisha kikao dha dharura mjini Jeddah, Saudi Arabia wakati huu ambapo Iran na kambi ya muqawama inajiandaa kutoa majibu makali kwa Israel kutokana na vitendo vya kigaidi vya utawala wa Kizayuni. Ali Bagheri, Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, jana Jumatano asubuhi aliondoka mjini Tehran kuelekea Jeddah, akiongoza ujumbe wa Iran kwa ajili ya kushiriki katika kikao hicho cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa OIC. Kikao hicho cha OIC ni cha kujadili matokeo mabaya ya jinai za Wazayuni dhidi ya wananchi wa Palestina na vilevile jinai ya utawala haramu wa Kizayuni ya kumuua shahidi Sheikh Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS. Jinai nyingine ya Israel ...

Kiwewe cha Wazayuni baada ya kuchaguliwa Yahya Sinwar kuwa mkuu mpya wa ofisi ya kisiasa ya HAMAS

Image
  Kiwewe cha Wazayuni baada ya kuchaguliwa Yahya Sinwar kuwa mkuu mpya wa ofisi ya kisiasa ya HAMAS Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imemteua Yahya Sinwar kuwa Kiongozi wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati hiyo ya muqawama, kujaza nafasi iliyoachwa wazi na hayati Ismail Haniyah. Shahidi Haniyah aliuawa kigaidi na utawala wa Kizayuni hapa mjini Tehran tarehe 31 Julai, siku moja baada ya kuhudhuria hafla ya kuapishwa Rais mpya wa Iran, Masoud Pezeshkian. Kuchaguliwa Yahya Sinwar kuwa mkuu mpya wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) kumeibua mshangao, hofu na wahaka mkubwa kwa utawala wa Kizayuni. Yahya Ebrahim Sinwar ndiye mwanzilishi wa idara ya usalama ya Hamas, iliyopewa jina la "Majd", inayoshughulikia kesi za usalama wa ndani. Utawala wa Kizayuni ulifeli katika shambulio la kigaidi la kutaka kumuua Sinwar. Kuchaguliwa Yahya Si...

Uingereza katika dimbwi la ghasia za siasa kali za wafuasi wa mrengo wa kulia

Image
  Uingereza katika dimbwi la ghasia za siasa kali za wafuasi wa mrengo wa kulia Serikali ya Uingereza imeitisha kikao cha dharura ikiwa ni radiamali ya kuenea ghasia na vitendo vya utumiaji mabavu vya wafuasi wa mrengo wa kulia dhidi ya wahamiaji na Waislamu. Keir Starmer Waziri Mkuu wa Uingereza amelaani shambulizi dhidi ya hoteli moja ya wakimbizi huko Rotherham na kusema kuwa atashughulikia machafuko hayo "kwa kiwango cha juu kabisa cha sheria". Waziri Mkuu wa Uingereza ametaja machafuko hayo kuwa ni vitendo vya "makundi ya kihuni ya watu wa mrengo wa kulia" na kusema "watajuta” kwa vitendo vyao hivyo. Vitendo vya Uasi na ghasia za makundi ya kibaguzi na yanayopinga wahajiri na Waislamu vimeongezeka katika wiki ya karibuni katika miji kadhaa ya Uingereza. Mashambulizi dhidi ya misikiti, maeneo ya ibada ya Waislamu, makazi ya raia, vituo vya biash...

Utendaji wa kiuadui wa Israel dhidi ya Iran na muqawama na athari hasi za kijamii katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu

Image
  Utendaji wa kiuadui wa Israel dhidi ya Iran na muqawama na athari hasi za kijamii katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu Hali na mazingira ya kijamii katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) yapo kwa namna ambayo vitisho vya nje vitakuwa na uharibifu mkubwa na matokeo mabaya kwa jamii hiyo. Jumatano iliyopita na katika kitendo kingine cha jinai, utawala wa kigaidi wa Kizayuni ulimuua shahidi Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS. Jinai hiyo ya kinyama ya Israel ilitekelezwa hapa mjini Tehran. Baada ya jinai hiyo, Kiongozi wa Muadhamu Mapinduzi ya Kiislamu alitangaza katika ujumbe wake akisema: Utawala wa Kizayuni ambao ni mtenda jinai na ni utawala wa kigaidi, umemuua shahidi mgeni wetu kipenzi kwenye nyumba yetu na kututia majonzi makubwa, hivyo utawala huo umejiandalia mazingira ya kuadhibiwa v...

Takwa la Baghdad la kuondolewa wanajeshi wa Marekani kutoka Iraq

Image
  Takwa la Baghdad la kuondolewa wanajeshi wa Marekani kutoka Iraq Kamisheni ya Usalama na Ulinzi ya Bunge la Iraq imetoa mwito wa kuainishwa ratiba na jedwali la kuondoka wanajeshi wa Marekani kutoka katika ardhi ya nchi hiyo ya Kiarabu Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iraq, Kamisheni ya Ulinzi na Usalama ya Bunge la Iraq imekosoa kuendelea kuwepo vikosi vya kigeni nchini humo na kusisitiza ulazima wa kuandaliwa ratiba ya kuondoka askari wa kigeni kutoka Iraq. Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, iwapo vikosi vamizi vitaendelea kuweko nchini Iraq, basi yamkini hali ikatoka nje ya udhibiti. Tangu mwaka 2014, takriban wanajeshi 2,500 wa Marekani wamekuwepo nchini Iraq kwa kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi la Daes, na wanajeshi hao wamesambazwa katika vituo vitatu kuu: Ain al-Asad mjini Anbar, Harir mjini Erbil, na Camp Victory jirani na Uwanja wa Ndege wa Kimataif...

Iran na Russia katika mkondo wa kuimarisha ushirikiano

Image
  Iran na Russia katika mkondo wa kuimarisha ushirikiano Jumatatu ya jana tarehe 5 Agosti, Katibu wa Baraza la Usalama la Taifa la Shirikisho la Russia  aliwasili mjini Tehran kwa lengo la kuimarisha maingiliano na kuchunguza masuala ya kieneo, kimataifa na uhusiano wa pande mbili. Katika muendelezo wa ushirikiano wa kistratijia kati ya Tehran na Moscow, ujumbe wa ngazi ya juu wa Russia ukiongozwa na "Sergei Shoigu", Katibu wa Baraza la Usalama la Taifa la Russia uliwasili Tehran Jumatatu kwa mwaliko wa mwenzake wa Iran Ali Akbar Ahmadian.  Akiwa hapa mjini Tehran, Shoigu amekutana na rais, mkuu wa majeshi na mwenyeji wake Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran. Katika mazungumzo hayo, kulijadiliwa masuala mbalimbali kama ushirikiano mpana wa pande mbili na uimarishaji wake kuanzia usalama hadi mipango ya kibiashara na kiuchumi, pamoja na masuala mbali...

Rais Maduro wa Venezuela aituhumu WhatsApp kwa kufanya ujasusi

Image
  Rais Maduro wa Venezuela aituhumu WhatsApp kwa kufanya ujasusi Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ameituhumu WhatsApp kuwa ni mfumo unaofanya ujasusi, na hivyo amewashauri watu kuachana na WhatsApp na kutumia mitandao mingine. Akizungumza ikulu mjini Caracas katika mkutano na wawakilishi wa sekta za uvuvi na kilimo za Venezuela, Rais Nicolas Maduro amesema, "WhatsApp iliwapatia walanguzi wa dawa za kulevya wa Colombia orodha ya watu wanaotumia mtandao huo huko Venezuela na kisha walanguzi hao walifanya kazi ya ujasusi kwa miezi kadhaa."  Rais wa Venezuela ameongeza kusema, mtandao huo wa  kijamii ulitumiwa kwa ajili ya vita vya kisaikolojia, kutoa vitisho kwa mamilioni ya viongozi, kuzitishia jamii mbalimbali, viongozi wa serikali za mitaa, familia za wanajeshi na polisi, wanariadha, wasanii na mtu yeyote ambaye hakuunga mkono ...

Muhammad Eslami: Sera za milango wazi zipo katika ajenda ya kazi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Image
  Muhammad Eslami: Sera za milango wazi zipo katika ajenda ya kazi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia ya Iran amesema kuwa nchi za Magharibi zinaituhumu Iran kuwa inaficha sekta yake ya nyuklia, ilhali Tehran inatekeleza sera za milango wazi katika ajenda yake. Muhammad Eslami amesema kuwa nchi za Magharibi zinapinga maendeleo ya sekta ya nyuklia ya Iran na kwamba  hivi sasa dawa aina 60 zinazalishwa nchini Iran kwa kutumia teknolojia ya nyuklia, na dawa nyingine 20 katika ziko katika majaribio ya kimatibabu.  Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia ya Iran alieleza haya jana Alhamisi katika Mkutano wa Taifa kuhusu Nafasi na Matumizi ya Teknolojia ya Nyukia katika Mfumo wa Afya". Eslami pia aligusia jinai kubwa na za kikatili zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia wa Palestina wasio na ulinzi ...

Iran: Kuchaguliwa al Sinwar kunadhihirisha matumaini, umoja na nguvu ndani ya Hamas

Image
  Iran: Kuchaguliwa al Sinwar kunadhihirisha matumaini, umoja na nguvu ndani ya Hamas Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa kuchaguliwa Yahya al Sinwar kuwa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) kunaonyesha umoja na uwezo wa harakati hiyo ya muqawama mkabala wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Baada ya kuuawa shahidi Ismail Haniyeh, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imemchagua Yahya Ibrahim al Sinwar kuwa Mkuu wa Ofsi ya Kisiasa ya harakati hiyo.  Yahya Sinwar, Mkuu mpya wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas  Ismail Haniyeh, aliyekuwa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas, na mlinzi wake waliuawa shahidi alfajiri ya Jumatano Julai 31 mwaka huu katika shambulio la kigaidi alipokuwa Tehran kushiriki hafla ya kuapishwa rasmi Rais mpya wa Iran.  Shirika la Habari la Iiran (IRNA) limeripoti kuw...

Palestina yaitaka ICC kumkamata Smotrich baada ya kutoa wito wa kuuawa Wapalestina mil. 2 kwa njaa

Image
  Palestina yaitaka ICC kumkamata Smotrich baada ya kutoa wito wa kuuawa Wapalestina mil. 2 kwa njaa Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kutoa hati ya kukamatwa Waziri wa Fedha wa Israel, Bezalel Smotrich, kwa sababu ya wito wake wa kuwaua kwa njaa Wapalestina milioni mbili huko Gaza. Ombi hili la serikali ya Palestina limetolewa baada ya vita vya Israel, vinavyoungwa mkono na Marekani, vinavyoendelea kwa zaidi ya miezi 10, kuua na kujeruhi zaidi ya Wapalestina 131,000, wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake, na wengine zaidi ya 10,000 wametoweka. Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imeyataja matamshi ya Bezalel Smotrich kuwa ni kielelezo cha sera za mauaji ya kimbari na kueleza kuwa matamshi hayo hayakulaaniwa na serikali ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. Pia imesisitiza kwamba alichosema Smotrich ni...

Watu 26 wahukumiwa kifo Kongo DR kwa 'jinai za kivita'

Image
  Watu 26 wahukumiwa kifo Kongo DR kwa 'jinai za kivita' Watu wasiopungua 26 wamehukumiwa kifo na mahakama ya kijeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya kupatikana na hatia katika mashitaka matatu yaliyokuwa yakiwakabili. Miongoni mwa waliohukumiwa kifo katika faili hilo ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (CENI), Corneille Nangaa Yobeluo, na wapambe wake. 26 hao walikuwa wanakabiliwa na mashitaka ya 'kula njama dhidi ya dola', jinai za kivita pamoja na kujihusisha na harakati za uasi. Mawakili wa washtakiwa hao wamesema hawakupewa muda wa kutosha wa kujenga hoja za kuwatetea wateja wao. Kati ya watu hao 26 waliopatikana na hatia, 21 wametoroka nchi, akiwemo Nangaa, ambaye ni kiongozi wa Muungano wa Mto Congo "Alliance Fleuve Congo" (AFC). Hukumu hiyo imetolewa siku chache baada ya ...

Madhara na uharibifu wa kinyama unaofanywa na Wazayuni katika mauaji ya kimbari ya Wapalestina

Image
  Madhara na uharibifu wa kinyama unaofanywa na Wazayuni katika mauaji ya kimbari ya Wapalestina Utawala wa Kizayuni wa Israel haujajiwekea mipaka yoyote katika mauaji ya halaiki na ya kimbari unayofanya dhidi ya wananchi wa Palestina. Askari wenyewe wa jeshi la utawala huo dhalimu wamekuwa wakikiri waziwazi na bila ya hofu kwamba wanawaua makusudi Wapalestina wasio na ulinzi wa Ukanda wa Ghaza. Katika mahojiano na televisheni ya CNN, baadhi ya askari walioamua kuacha kazi katika jeshi la utawala bandia wa Israel wameeleza kuwa, wamechoshwa na mbinu za kivita za kinyama zinazotumiwa na jeshi hilo huko Ghaza na kwamba hawakuweza kuustahamili uharibifu mkubwa uliofanywa wa kiwango walichoshuhudia katika eneo hilo.   CNN imetayarisha ripoti kuhusiana na suala hilo inayoonyesha upeo wa juu kabisa wa ukatili na jinai zilizofanywa na Wazayuni. A...

Sergei Shoigu: Ushirikiano wa Tehran na Moscow unaongezeka

Image
  Sergei Shoigu: Ushirikiano wa Tehran na Moscow unaongezeka Katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia amesema kuwa ushirikiano kati ya Tehran na Moscow unaendelea kupanuka. Sergei Shoigu amehojiwa na televisheni ya Russia 24 na kueleza kuwa ushirikiano wa Tehran na Moscow unaendelea kuimarika na kwa kasi kubwa katika nyanja zote.  Shoigu ameongeza kuwa, katika mazungumzo aliyofanya hapa Tehran na Rais Masoud Pezeshkian na Ali Akbar Ahmadian Katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Iran wamebadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa pande mbili na pia hali ya mambo ya Syria na Lebanon.  Mazungumzo kati ya Sergei Shoigu na Rais Masoud Pezeshkian wa Iran mjini Tehran  Katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia pia ameshiria tukio chungu la kuuliwa kigaidi Ismail Haniyeh Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas mjini Tehran na kueleza ku...

Katika miezi tisa iliyopita Yemen imeshambulia meli 170 za Marekani na Wazayuni

Image
  Katika miezi tisa iliyopita Yemen imeshambulia meli 170 za Marekani na Wazayuni Aug 08, 2024 06:32 UTC Tovuti ya habari ya Yemen imetangaza katika ripoti yake kuwa katika kipindi cha miezi tisa iliyopita vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vimezishambulia meli 170 za Wamarekani na Wazayuni.  Almasirah imeeleza katika ripoti yake iliyochunguza operesheni zilizofanywa na vikosi vya ulinzi vya Yemen kati ya Novemba 2023 hadi Julai mwaka huu kwamba katika operesheni hizo, vikosi hivyo vimezilenga meli zipatazo 170 zenye uhusiano na adui Mzayuni.   Kwa mujibu wa ripoti hiyo, meli 41 kati ya zilizopigwa zilikuwa za adui wa Kizayuni, meli 72 za Marekani na meli 12 zilikuwa za Uingereza.   Ripoti hiyo imeongeza kuwa, kati ya hizo zote, karibu meli 45 zimeshambuliwa na jeshi la Yemen kutokana na kukiuka marufuku ya kuingia katika bandar...

UN: Waliowafanyia unyama mahabusu wa Kipalestina katika jela za Israel wawajibishwe

Image
  UN: Waliowafanyia unyama mahabusu wa Kipalestina katika jela za Israel wawajibishwe Aug 08, 2024 07:33 UTC Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) amesema lazima kuwepo na uwajibishaji dhidi ya ukiukaji wa haki Wapalestina wanaoshikiliwa katika magereza ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Philippe Lazzarini ameeleza hayo katika ujumbe alioweka kwenye mtandao wa X na kusisitiza kwa kusema: "ubinadamu uko katika hali mbaya zaidi". Lazzarini amesema UNRWA imeguswa na  "mienendo isiyo ya kibinadamu" waliyofanyiwa mahabusu Wapalestina mnamo mwezi Aprili katika vituo vya mahabusu vya Israel.   Akiashiria ripoti ya hivi karibuni ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kuhusu vitendo hivyo pamoja na ripoti ya Kituo cha Habari cha Israel cha Haki za Binadamu katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu (B'tsele...

OIC yasema, Israel 'inabeba dhima kamili' ya mauaji ya Kiongozi wa HAMAS Ismail Haniya

Image
  OIC yasema, Israel 'inabeba dhima kamili' ya mauaji ya Kiongozi wa HAMAS Ismail Haniya Aug 08, 2024 06:32 UTC Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imeulaumu utawala wa Kizayuni wa Israel kwa shambulizi la kigaidi lililomuua Ismail Haniya Mkuu wa Tawi la Kisiasa la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS wiki iliyopita nchini Iran, ambayo Tehran imeapa kuyalipizia kisasi. Mbali na kulaani mauaji hayo, taarifa iliyotolewa jana Jumatano baada ya kikao cha dharura cha jumuiya hiyo yenye wanachama 57 kilichofanyika nchini Saudi Arabia imesema "inaibebesha Israel, utawala unaokalia ardhi kwa mabavu, dhima kamili ya shambulio hilo ovu sana", ambalo imelitaja kuwa ni "ukiukaji mkubwa" wa mamlaka ya kujitawala ya Iran. Kikao cha dharura cha OIC mjini Jeddah kimeitishwa kwa wito uliotolewa na Iran na Palestina. Image Caption ...

Ofisi ya Kudumu ya I.R.Iran UN: Iran itaifanya Israel ijutie uchokozi wa kigaidi iliofanya

Image
  Ofisi ya Kudumu ya I.R.Iran UN: Iran itaifanya Israel ijutie uchokozi wa kigaidi iliofanya Aug 08, 2024 07:05 UTC Ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa imesema Tehran itaufanya utawala wa Kizayuni wa Israel ujutie kitendo cha uchokozi wa kigaidi uliofanya hivi karibuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu uliopelekea kuuawa shahidi kiongozi mkuu wa Hamas, Ismail Haniya. Ofisi hiyo ya uwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika UN ilitoa kauli hiyo jana Jumatano wakati wa kujibu masuali kuhusu madai kwamba Tehran inaweza ikafuta kisasi chake ikiwa Tel Aviv itafikia makubaliano na Hamas ambayo yataleta suluhu katika vita vinavyoendelea vya utawala huo vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Ghaza.   "Tumekuwa tukifuatilia vipaumbele viwili kwa wakati mmoja," imeeleza ofisi hiyo ya uwakilishi wa Iran katika Umoja...